Bwana ajapo, ndugu, Bwana ajapo!
Itakuwaje na sisi, Bwana akija?
2. Atavikwa vizuri sana,taji badala ya miiba;
Kweli tokeo la fahari Bwana ajapo.
3. Kwa fufaha awakubali wenye mavazi ya arusi;
Tu wa heri tukimridhisha Bwana ajapo.
4. Kutakuwako na utengo: watalia waliomwasi;
Cha kutisha kitambo kile Kristo ajapo!
5. Mfalme utupe neema sisi tunapokungojea
Tusiogope kukuona ujapo Bwana.
173. Hatujui Saa - We Know Not the Hour
1. Hatujui sa-a ya kuja kwwa Bwana, Lakini dakiki zasema karibu
Atakporudi,--lakini kwa kweli Hatujui sa-a.
Atakuja, kwa vile tukeshe;
Atakuja Mwokozi, Aleluya!
Atakuja kwa fahari yu Baba yake,--
Hatujui sa-a.
2. Pana nuru kwao wapendao haki, pana kweli katika chuo cha Mungu;
Unabii hufundisha kuja kwake,--Hatujui saa.
3. Tutakesha na tutaomba daima, Tutafanya kazi mpaka akija,
Tutaimba na tutasoma ishara,--Hatujui saa.
174. Tukimngojea - We Know not the Time when He Cometh
1. Sijui atakapokuja,
Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari,
Ili ajapo atukute;
Tuwe tukimngoja Yeye.
Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu - - - kimngojea - - - a,
(kukesha, tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.
Nakesha, nakungojea.
175. Uso Kwa Uso - Face to Face
1. Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele nitamwona Mwokozi.
Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.
2. Sasa siwezi kujua jinso alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.
3. Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.
4. Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;
Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.
176. Ati Tuonane Mtoni? - Shall we Gather at River
1. Ati twonane mtoni? maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika kule mtoni penye kiti cha Mungu.
2. Tukitembea mtoni na Yesu mchunga wetu,
Daima tu ibadani usoni pake kwetu.
3. Tukisafiri mtoni tutue ulemeao,
Wema wa Mungu yakini: una taji na vao!
4. Kwang'ara sana mtoni cha Mwokozi ni kioo,
Milele hatuachani tumsifu kwa nyimbo.
5. Karibu sana mtoni, karibu tuatawasili,
Mara huwa furahani na amani ya kweli.
177. Kazi Yangu Ikiisha - When my Life-work is Ended
1. Kazi yangu ikisha, nami, nakiokoka,
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi; nivukapo ng'amboni
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Nitamjua, nitamjua,
Nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa alama za misumari.
2. Kuona uso wake utanipa furaha,
Furaha isiyo ya kukomesha;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyo nipa pahali mbingini.
3. Nao walio kufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4. Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi awla huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele: lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
178. Ukingoni Mwa Yordani - On Jordan's Stormy Banks
1. Ukingoni mwa Yordani ninaangalia
Bara nzuri ya Kaanani, ninayotamani.
Tutakaa pamoja na Yesu,
Katika pwani yenye raha;
Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo,
Milele hata milele.
2. Bara ile ina nuru, nuru ya milele;
Kristo, Jua, hutawala, hufukuza giza.
3. Nitapafikia lini na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba. Na kumwona uso?
4. Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa;
Siyaogopi mawimbi katika Yordani.
179. Watafurahi - O There'll Be Joy
1. Wavunaji watafurahi, pale watakapo rudi,
Wakiyaleta mavuno hata Yerusalemu.
Furaha wataipata, furaha hata milele,
Furaha, wataipata, wakati wa mavuno.
2. Na siku ile tutaimba, kumshukuru na kumsifu
Bwana Yesu Jumbe wetu, kule Yerusalemu.
3. Wavunaji watafurahi makaoni mwa milele
Yaliyowekwa tayari kule Yerusalemi.
180. Pana Mahali Pazuri Mno - There's a Land
1. Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu angoja pale,
Amepanga makao yetu.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng'ambo pale.
2. Tutaimba pale kwa moyo
Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.
3. Kwa Baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake
Na baraka anazotupa.
Nyimbo za kristo 141-160
141. Chini Ya Msalaba - Beneath the Cross of Jesus
1. Chini ya msalaba Nataka simama;
Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema;
Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili,
Tatua mziho wangu Wakati wa hari.
2. Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili;
Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli;
Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani,
Msalaba umekuwa ngazi ya mbinguni.
3. Na Yesu Msalabani Walimkimea,
Alikufa niokoke Niliyepotea:
Naona ajabu sana Ya manbo mawili
Jinsi alivyonipenda Nisiyestahili.
4. Atakayeonana Na Yesu mbinguni,
Njia yake aanzapo Ni Msalabani;
Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana,
Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.
142. Nasikia Sauti Yako - I hear Thy Welcome Voice
1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.
Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.
2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.
3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.
4. Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.
143. Naamini - Father, I Stretch My Hands
1. Baba sina msaada ila kwako pekee;
Kama kwangu ungefichwa, Nifanyeji, Baba?
Sasa hivi naamini Yesu alikufa,
Aliimwaga damu yake, Nitoke dhambini.
2. Naamini mwana wako Nipe nguvu zako;
Nijazie mahitaji, katika saa hii.
1. Ni wako Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea.
Bwana vuta, (vuta) nije nisongee
Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee
Pa damu ya thamani.
2. Niweke sasa nikatumike kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.
3. Nina furaha tele kila saa nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.
145. Namtaka Bwana Yesu - Take The World
1. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Dunia hunidanganya; yesu yu mwaminifu.
Rehema ni ya ajabu! Pendo bila kipimo!
Wokovu mkamilifu, Amana ya uzima.
2. Ulimwengu siutaki, Namtaka Bwana yesu;
Kati ya dhoruba kali Yeye wimbo mtamu.
3. Ulimwengu siutaki, namtaka Bwana yesu;
Safarini duniani Yeye furaha yangu.
1. Kuwa wake Yesu, je! Ni kusudi lako?
Ungeenda naye njia nyembamba?
Unataka aubebe mzigo wako?
Awe Mwongozi wako.
Uwezo wake unakutosha
Na danu yake itakusafi;
Kwa vile ukubali ni bora
Afanye mapenzi yake nawe
2. Unataka kutika unapokwita?
Kupata amani kwa kumpa vyote?
Wataka uwezo usianguke kamwe?
Awe Mwongozi wako.
3. Wataka raha katiak ufalme wake?
Ungeshinda kwa majaribu yote?
Ungefanya kazi yake vizuri sana?
Awe Mwongozi wako.
150. Hasha Maneno Mabaya Yasitoke - Angry Words! Oh, Let them Never
2. Pendo ni mtakatifu; Urafiki; mzuri:
Visiharibike mara kwa kunena vibaya.
3. Tusinene kwa hasira, inazaa huzuni,
Pendo lako ee mwokozi, Inatosha tushindi.
151. Huniongoza Mwokozi - He Leadeth Me
1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.
Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozae.
2. Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote, yupo nami siku zote.
3. Mkono akinishika kamwe sitanung'unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.
4. Nikiisha kazi chini sita kimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.
152. Karibu Na Wewe, Mungu Wangu - Nearer, My God, to Thee
1. Karibu na wewe, Mungu wangu:
Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.
2. Mimi nasafiri duniani,
Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.
3. Yote unipayo yanivuta;
Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.
4. Na kwa nguvu zangu nikusifu;
Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe;
Karibu zaidi, Mungu wangu.
5. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu
Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe,
Karibu zaidi, Mungu wangu.
153. Fikira Moja Tu - One Sweetly Solemn Thought
1. Fikira moja tu
Hurejea tena
Nimekaribia mbingu
Zaidi ya jana.
Karibu na kwetu mbingu,
Karibu na kwetu sasa,
Nikwone karibu.
2. Karibu na kwetu
Na kwenye makao;
Kiti cha enzi cha Mungu,
Pahali pa mto.
3. Kamilisha Yesu,
Kuamini kwangu;
Nikifika mwisho wangu,
Nikwone karibu.
154. Yanipasa Kuwa Naye - I Must Have The Saviour With Me
1. Yanipasa kuwa naye, Mwokozi Bwana wangu,
Akiwa karibu nami, napata nguvu kweli.
Moyo hauogopi, wala kitikisika.
Nitakwenda apendapo. Kwa kuwa anilinda.
2. Yanipasa kuwa naye, kwani nategemea;
Anaweza kufariji na maneno matamu.
3. Yanipasa kuwa naye maisha yangu yote;
Yakiwapo majaribu na mashaka yo yote.
4. Yanipasa kuwa naye katika njia zangu;
Macho yake yaongoza hatua zangu zote.
155. Njiani Huniongoza - All the Way my Saviour Leads Me
1. Njiani huniongoza. Yesu wangu, Mwokozi;
Rehema hatapunguza, Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana Duniani daima;
Nijaposumbuka sana, Yeye hutenda vyema,
2. Njiani huniongoza Hupunguza matata;
Nikiugua hupoza, Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu Hunibubujikia.
3. Njiani huniongoza Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza Kwake Baba yangu juu.
Nikivikwa kutokufa, Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa: "Kweli ni Kiongozi."
156. Uniongoze, Yehova - Guide Me, O Thou Great Jehovah
1. Uniongoze, Yehova, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, u hodari, 'Nilinde kwa mkono.
Unitunze, unilinde, Unionyeshe njia!
2. Na kisima cha uzima, Maji ya utabibu,
Fungua kwa moyo wangu, Ninywe na kuponyeka!
Uninyweshe, unilishe, Hata nimetosheka.
3. Wakati wa kuuvuka, Ule mto Yordani,
Hofu yangu ufariji, 'Nione uso wako.
Nyimbo shangwe, nyimbo shangwe, Nitaimba daima.
157. Mfalme Yu Mlangoni - The Coming King
1. Mfalme yu mlangoni, Ndiye aliyetufia;
Mara wote wampendao atawakusanya.
Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama;
Anakuja, anakuja, Kuja kwake karibu.
2. Dalili za kuja kwake Zinazidi kutimizwa;
Karibu wateule watamlaki Bwana.
3. 'Sitafute duniani amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi dhambi kuondoa.
4. Tutakaa na Mwokozi Makaoni ya milele;
Daima tutafurahi kuwa watu wake.
158. U Mwendo Gani Nyumbani? - How Far From Home?
1. U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha, mahe kaibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.
2. Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.
3. Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanye kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.
4. Siyo mbali na nyumbani! Fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.
159. Anakuja Upesi - How Sweet are the Tidings
1. Anakuja upesi, Yesu Bwana wetu, Msafiri mbali na kwao;
Alisema dhahiri, "Nitakuja tena"; Amina; na uje, E Bwana.
Yuaja, Yesu atarudi sasa; Anakuja duniani.
Wasafiri wote watapumzika Yesu anaporudi tena.
2. Makaburi yote wafu wanapolala Yatafunguliwa tena;
Na mamilioni pale wataondoka tena, Wasione machozi kamwe.
3. Hatutatengana na hao tena huko; Nyimbo nzuri tutaimba.
Watakusanyika 'toka kila kabila, Miguuni pa Mwana-kondoo.
4. Aleluya Amin! Aleluya tena! Upendo wake unashinda!
Tutamsifu milele, hata tutashangaa, Jinsi alivyo tukomboa.
160. Watakatifu Kesheni - Watch, Ye Saints
1. Watakatifu kesheni, nguvu za mbingu zagonga;
Washeni taa tayari kwa kurudi kwake Bwana.
Yuaja, Yesu Mfalme, Yuaja myenye fahari,
Yesu yuaja enzini. Karibu Yesu, uje.
2. Piga mbiu, tangazeni habari ya ukombozi,
Ya mponya wa upendo nayo nguzu za samaha.
3. Falme nyingi zaangushwa, Panda ya saba hulia;
Tangaza neema yake kabla ya kupita saa.
4. Mataifa yapotea, nchi zajaa uchungu:
Kistro anaharakisha, Unabii unatimizwa.
5. Wenye dhambi njoni sasa, Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema, kitambo muda waisha.
Nyimbo za kristi 121-140
121. Katika Wenye Dhambi - Chief Of Sinners
1.Katika wenye dhambi Ndimi mkuu wao—
Ila yesu akaja, Kwa dhanbi alikufa,
Akamimina damu Niupate uzima.
4. Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamani nitii pia.
5. Nitamfurahia na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia.
129. Kumtegemea Mwokozi - 'Tis So Sweet To Trust
1. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake nimeoshwa kamili.
2. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa
Kuamini damu yake nimeoshwa kamili.
3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima napata, uzima na amani.
4. Nafurahi kwa sababu nimekutegema;
Yesu, M-pendwa, Rafiki, uwe nami dawamu.
130. Yesu Kwetu Ni Rafiki - What A Friend We Have In Jesus
1. Yesu kwetu ni rafiki, hwambiwa haja pia;
Tukiombawka Babaye, maombi asikia;
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya;
Kama tulimwomba Mungu, dua atasikia.
2. Una dhiki na maonjo? Unamashaka pia?
Haifai kufa moyo, dua atasikia.
Hakuna mwingine Mwema, wa kutuhurumia:
Atujua tu dhaifu: Maombi asikia.
3. Je, hunayo hata nguvu, Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa. ujaporushwa pia.
Watu wange kudharau, wapendao dunia.
Hukwambata mikononi, dua atasikia.
131. Baba Anilinda - I Trust In God
1. Namtegemea Mungu niwapo
Humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda.
Baba wa mbinguni anilinda.
Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini) Baharini
Moyo Wangu (moyo wangu.) aulinda (aulinda).
Baba wa mbinguni anilinda.
2. La waridi alinawirisha,
Na huyo tai juu angani,
Nami kweli ananilinda,
Baba wa mbinguni anilinda.
3. Tunduni mwa simba namwamini,
Kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni,
Baba wa mbinguni anilinda.
4. Bondeni mwa giza na upweke,
Mchunga wangu yuanilinda,
Kwa upole aniongoza.
Baba wa mbinguni anilinda.
131a. Kwa Mahitaji Ya Kesho - Lord for Tommorrow and It's Needs
1. Kwa mahitaji ya kesho, Sian ombi;
Unilinde nisitende Dhambi leo;
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, leo hivi.
2. Ningefanya kazi sawa Na kuomba;
Ningekuwa mtu mwema Kila saa;
Mapenzi yako nifanye, Na kutii;
Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.
3. kama keo ningekufa Kwa ghafula,
Nitegemee ahadi Zako Bwana.
Kwa mahitaji ya kesho sina ombi;
Uniongoze, Nishike Leo hivi.
132. Bwana Ni Mchunga - The Lord is My Sherpherd
1. Bwana ni Mchunga, Sitahiji;
Majani mabichi mlisho yangu.
Ananinywesha maji Matulivu;
Atanirudisha nikipotea.
2. Nipitapo bondeni mwa mauti
U mlinzi wangu—sitaogopa;
Fimbo lako latoshakunilinda;
Ukinifariji sina hasara.
3. Kati ya mateso mea waandaa,
Na kikombe changu kinafurika;
Umenipaka kichwani mafuta;
Nitaulizaje zaidi kwako?
4. Wema na fadhili zinifuate
Siku zangu zote hata milele;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
Katika ufalme wa pendo lake.
133. Po Pote Na Yesu - Anywhere With Jesus
1. Po Pote na Yesu nina furaha;
Anitumako Yesu ndiyo raha.
Asipokuwako hapanifai,
Akiwapo Yesu, mimi sitishwi.
Po pote, po pote, sina mashaka:
Po pote na Yesu naweza kwenda.
2. Akiwapo yesu, si peke yangu;
Na nijapotupwa, akali wangu;
Ajaponiongoza njia nbaya,
Niwapo na Yesu nashukuria.
3. Akiwapo yesu naweza lala,
naweza pumzika hata kiyama;
Kisha nitakwenda kwake milele,
akiwapo Yesu furaha tele.
134. Tafuta Daima Utakatifu - Take Time to be Holy
1. Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.
3. Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.
4. Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.
135. Kwa Maombi Nachangamka - Sweet Hour Of Prayer
1. Saa heri ya maombi, sasa kwako tunarudi,
Sumbuku ya kuondoa, shida zitu na pungufu.
Taabuni mara nyingi, roho zetu zimepona,
Mashakani tumeshinda, wakati wa saa tamu.
2. Saa heri ya maombi, Twapelika dhiki zetu
Kwake aliyeahidi kubariki wenye haja.
Huagiza tumwendee, tutegemee neno lake,
Hivyo tumwekee yote, wakati wa saa tamu.
3. Saa heri ya maombi, tutazidi kuingia
Bomani mwetu na ngome, hata tuishapo mwendo.
Yesu atatusikea, tutamtafuta daima,
Na tutakapolutana tutamwona—saa tamu!
136. Niwe Kama Yesu - Teach Me Father
1. Unifundishe, Baba; Ile njia ya sala;
Uniendeshe sana, Niwe kama Yesu.
Niwe kama Yesu, Niwe kama Yesu,
Uniongoze, Baba; Niwe kama Yesu.
2. Unipe pendo, Baba, Watu kuwaokoa;
Nyumbani na mjini. Niwe kama Yesu.
3. Na unifahamishe, Wakati ndio mfupi;
Unibidishe, bwana, Niwe kama Yesu.
137. Saa Heri Ya Sala - 'Tis the Blessed Hour of Prayer
1. Saa heri ya sala tunapojidhili,
Kama tukija kwake yesu rafiki.
Tukiwa na imani kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana watapata raha.
Saa ya sala, iliyo heri;
Waliochoka sana watapata raha.
2. Saa heri ya sala, ajapo mwokozi,
Ili awasikie watoto wake.
Hutwambia tuweke miguuni pake
Mizigo yetu yote: tutapata raha.
3. Saa heri ya sala, wawezapo kuja
Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa;
Moyo wake mpole, atawarehemu;
Waliochoka sana watapata raha.
4. Saa heri ya sala tutakapopewa
Mibaraka ya roho, tukimwamini;
Kwa kuamini kweli hatutaogopa;
Waliochoka sana watapata raha.
4. Nijapoona ukiwa na mateso makali,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.
5. ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza nami nitaandana.
139. Uliniimbie Tena - Sing them over again
1. Uliniimbie tena, Neno la uzima;
Uzuri wake nione, Neno la uzima;
Neno hili zuri, lafundisha kweli:
Maneno ya uzima ni maneno mazuri,
Manemo ya uzima ni naneno mazuri.
2. Kristo anatupa sote, Neno la uzima:
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Latolewa bure, Tupate wokovu:
3. Neno tamu la Injili, neno la uzima;
Mwenye dhambi asikie Neno la uzima:
Litatutakasa, kwa haki ya Mwana:
140. Hivi Nilivyo Unitwae - Just as I am
1. Nitwae hivi nilivyo, umemwaga damu yako,
Nawe ulinyoniita, Bwana Yesu, sasa naja.
2. Hivi nilinyo; si langu kujiosha roho yangu;
Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, sasa naja.
3. Hivi nilivyo; sioni kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani, Bwana Yesu, sasa naja.
4. Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu;
Wewe ndiwe u tajiri, Bwana Yesu, sasa naja.
5. Hivi nilivyo, mimi tu, siwezi kujiokoa;
Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, sasa naja.
6. Hivi nilivyo; mapenzi yamenipa njia wazi;
Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, sasa naja.
Nyimbo za kristo 101-120
101. Yesu Akwita - Jesus Is Tenderly Calling Today
3. Usikie sauti Ya Bwana. (Uisikie)
Uyachague mambo Ya Bwana. (Mambo ya Bwana)
Ufungue mlango,
Usimwambie bado:
Jina lake tumai---- Yu Bwana. (Jina la Bwana)
4. Na ufungue moyo, Kwa Bwana (Fungulieni)
Utapewa msaada, Wa Bwana (Msaada wetu)
Uzuri utavikwa
Dhambi ataondoa,
Ukifungua moyo. Kwa Bwana (Fungulieni)
103. Njoni Kwangu - Softly and Tenderly
1. Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami;
Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.
"Njoni kwangu, Mliochoka, njoni:
Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, "uje kwangu"
3. Siku za maisha hupita hima, Hupita kwako, kwangu;
Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.
4. Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu;
Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.
104. Yesu Aliniita "Njoo" - I Heard the Voice of Jesus Say
1. Yesu aliniita, "Njoo Raha iko kwangu,
Kichwa chko ukilaze Kifuani mwangu"
Nilikwenda kwake mara, sana nilichoka;
Nikapata kwake raha Na furaha tena.
2. Yesu aliniita, "Njoo, Kwangu kuna maji;
Maji ya Uzima, bure, Unywe uwe hai."
Nilikwenda kwake mara na maji nikanywa;
Naishi kwake na kiu Kamwe sina tena.
3. Yesu aliniita, "Njoo, Dunia i giza,
Ukinitazama, nuru Takung'arizia.'
Nili kwenda kwake mara, Yeye jua langu,
Ni kila wakati mwanga Safarini Mwangu.
1. Mchungaji mpenzi hukuita uje
Katika zizi lake Panapo salama;
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake
Huita kwa moyo wa huruma, 'Uluyepotea uje kwangu';
Hivi kukungoja anadumu Bwana Yesu Mchunga.
2. Akatoa maisha kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu waje kwake sasa;
Tusijihatirishe; Kwake tu salama;
Sikia wito wake, Mchungaji wetu.
3. Tusikawie tena, adui shetani,
Kama Mbwa wa mwitu, atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.
106. Huna Kitu Kwa Yesu? - Nothing for Jesus
1. Ukitafuta mali, Huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki Huna wasaa kwa Yesu?
Ansa za kunia, Mambo yako ya raha
Haya unatafuta; Huna wasaa kwa yesu?
3. Sa-a ni za thamani, Kwake huna nafasi?
Wala hamfnyi bidii, Kwake hamnayo kazi?
Hamkufika kwao Waliomo shimoni
Na waliopotea? Kwake hamnayo kazi?
4. Na wazaa majani tu? Huna tunda kwa Yesu?
Mikono i mitupu, Huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala kazi yako kulipa;
Wala huna furaha Unapomwona Yesu?
107. Nipo Bwana, Nitume - Hark! The Voice Of Jesus
1. Sauti ni yake Bwana, "Kwenda, nani tayari"
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu amaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu "Nipo Bwana, nitume."
2. Kana huwezi safari Hata Nchi za mbali,
Pana watu karibuni Wasio mjua Yesu;
Kama huwezi kusema Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza Upendo wa mwokozi.
3. Ingawa huwezi kuwa Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu, Kuinua Mikono.
4. Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, "Hakuna kazi kwangu."
Kwa furaha anza kazi Ile akiyokupa,
Ukajibu mara moja "nipo Bwana, nitume."
108. Tumesikia Mbiu - We Have Heard a Joyful Sound
1. Tumesikia mbiu: Yesu huokoa;
Utangazeni kote, Yesu Huokoa.
Tiini amri hiyo: nchimi baharini,
Enezeni mbiu hii: Yesu huokoa.
2. Imba nawe askari: Yesu huokoa;
Kwa nguvu ya kombozi, Yesu huokoa;
Imbeni wenye shida, unapounwa moyo,
Na kaburini imba: Yesu huokoa.
3. Mawimbini uenee. Yesu huokoa.
Wenye dhambi jueni: Yesu huokoa;
Visiwa na viimbe, vilindi itikeni,
Na nchi shangilie: Yesu huokoa.
4. Upepo utangaze: Yesu huokoa.
Mataifa ya shangaa: Yesu huokoa;
Milimani, bondeni, sauti isikike
Ya winbo wa washindi: Yesu huokoa.
109. Anisikiaye - Whoever heareth
1. Anisikiaye, aliye yote, sana litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate, atakye na aje!
Ni "atakaye," Ni "atakaye";
Pwani hata bara, na litangae:
Ni Baba mpenzi alinganaye atakaye na aje!
2. Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema
Ndimi Njia, kweli, ndimi uzima: atakaye na aje!
3. Atakaye aje, ndiyo ahadi; atakaye hiyo haitarudi!
Atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.
110. Mlango Wazi - There is a Gate
1. Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu aneufungua Na hakuna kufunga.
Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?
2. Mlango hukaa wazi watu waokolewe:
Maskini ma matajiri Wa mataifa yote.
4. Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
'pendo la Yesu hushinda. Unainama kwake!
111. Tabibu Mkuu - The Great Physician
1. Tabibu mku-u huyu, Yesu mwenye huruma:
Atuletaye faraja : Yesu mwokozi wetu.
Imbeni, Malaika Sifa za bwana wetu;
Jina la pekee kwetu, ni la Yesu Bwana.
2. Mwana kondo-o msifuni Mwokozi:
Hatia zote na dhambi Huziondoa Yesu.
3. Hakuna jina jingine Linalofa-a sifa:
A-u kutufurahisha, Isipo kuwa lake.
1. Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema: "Nitazifuta zote."
3. Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili viwe vyako milele.
4. Kwa damu yake sasa amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.
116. Moyo Safi - One Thing I of the Lord Desire
1. Bwana ninataka hili, kwa kuwa nimechafuka,
Kwa moto au kwa maji unisafishe kabisa.
Unisafishe Mwokozi ndani, na nje, kwa moto—
Utakavyo: ili dhambi ife kwangu, ife kwangu.
2. Kupewa hekima yote, itakuwa tunu kubwa;
Lakini moyo safi ni, bora kwangu, bora kwangu!
3. Mpaka moyo ni safi siwezi kuyafahamu
Mambo mazuri ya mbingu, mambo mazuri ya mbingu.
4. Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako. 'taimba milele.
117. Wamwendea Yesu - Have You Been to Jesus?
1.Wamwendea Yesu kwa kusafiwa. Kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je, neema yake yatumwagiwa? Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe sana; waoshwa kwa damu ya Kondoo.
2.Wamwandana daima Mkombozi.Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa mavazi? Waoshwa kwa. Damu ya Kondoo?
3.Atakapokuja Bwana-arusi Uwe safi katika damu!
Yafae kwenda Mbinguni mavazi: Yaoshwa kwa damu ya kondoo?
4.Yatupwe Yalipo na takataka; Uoshawe kwa damu ya Kondoo:
Huoni kijito chatiririka Uoshwe kwa damu ya Kondoo?
118. Nilipotoka Kabisa - I've Wandered Far Away
1.Nilipotoka kabisa, sasa narudi
Nikakawia dhambini, Bwana narudi.
Narudi nyumbani: daima kwako.
Kwa upendo nipokee: Naja nyumbani.
2.Nikasusurika sana, sasa narudi
Mwenye uchungu natubu, Bwana narudi.
3.Nimechoka maovuni, sasa narudi;
Pendo lako lanivuta, Bwana narudi.
4. Ndilo tumaini langu, sasa narudi;
Yesu alinifilia, Bwana narudi.
5. Damu yake yanitosha, sasa narudi;
Unioshe kenyekenye, bwana narudi.
119. Alilipa Bei - I Hear the Saviour Say
1.Yesu anasema, "Wewe huna nguvu
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanangu.
Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, aliiondoa.
2. Bwana, nimeona Uwezo wako tu
Waweza 'takasa Mioyo michafu.
3. Sina kitu chema Kudai Neema,
Hivi nitafua Mavazi kwa damu.
4. Ninaposimama Juu ya mawingu,
Taji nitaweka Miguuni pa Yesu.
120. Msalaba wa Yesu - Jesus, Keep Me Near The Cross
1. Msalaba wa Yesu, Nikae karibu;
Pale pana chemchemi Ya kuponya dhambi.
Pale msalaba Msalaba wake,
Huo ni sifa yangu Kwa maisha yote.
2. karibu msalaba Nalitetemeka,
Pendo likaniona Likanirenemu.
3. Unikumbushe yesu, Nikuone pale;
Niupate upendo Na kuvutwa nao.
4. Karibu msalaba, Kwa kutegimea,
Kukesha na kungoja, Nitakaa pale.
Nyimbo za kristo 91-100
91. Kaa Nami - Abide with Me
1. Kaa nami, ni isiku tena;
Isiniache gizani, Bwana.
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.
2. Siku zetu hazakawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho kakikomi,
Isiye na mwisho kaa nami.
3. Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe? Bwana, kaa nami.
4. Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
5. Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote; kaa nami.
92. Magharibi Jua - Day is Dyding in the West
1. Magharibi jua limekwisha kushuka,
Mwezi na nyota sasa vinamsifu Muumba wa usiku.
Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.
2. Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni.
Utuhifadhi sisi, tufahamu gizani, U karibu.
3. Mapenzi yako makuu yawe nasi usiku,
Tuli usingizini, kucha vivyo roho Tushukuru.
4. Na utakapo kuja na nguvu kutawala,
Mungu wangu kubali kunichikua mimi Uliko juu.
Baba, Mwana, Roho, Mungu wetu,
Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu.
93. Jua La Rohoni Mwangu - Sun of My Soul
1. Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.
6. Asubuhi tutokapo, tukaribishe tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.
94. Po Pote Mashamba Yajaa - Far And Near The Fields
1. Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu,
Po pote yang'aa meupe bondeni na nyandani.
Mwenye mavuno, twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.
2. Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.
3. Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.
95. Zileteni Zaka Kwa Hazina - Bring Ye All The Tithes
1. Sikieni neno la Mungu Wetu, Zileteni zaka kwa hazina
Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja.
Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo;
Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafsi ya kupewa.
2. Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina
Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utakapo barikiwa.
3. Je! Unakasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina
Uzilete kama alivyosema, Ndipo utakapo barikiwa.
4. Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani;
Usadiki ahadi zake zote, ndipo utakapo barikiwa.
5. Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani
Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.
96. Mali Yako Sasa - We Give Thee But Thine Own
1. Mali yako sasa, Bwana, tutatoa;
Hatuna yaliyo yetu, Yote ni vipaji.
2. Sisi watumishi, Twaungama deni;
Tunge irudisha kwake, Iliyo ya Bwana.
3. Utusaidie, Upendo kujua,
Kwa ajili yao wote Walio gizani.
4. Neno tumaini na kutegemea:
Kwamba lote tufanyalo, Tulifanye kwako.
97. Sioshwi Dhambi Zangu - What Can Wash Away My Sin?
1. Sioshwi dhambi zangu bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu bila damu yake Yesu.
Hakuna kabisa dawa ya makosa
Ya Kututukasa ila damu yake Yesu.
2. La kunisafi sina ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena ila damu yake Yesu.
3. Sipati patanishwa bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, bila damu yake Yesu.
4. Sipati tumaini bila damu yake Yesu,
Wema wala amani bila damu yake Yesu.
5. Yashinda ulimwengu, iyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, iyo, damu yake Yesu.
98. Nilikupa Wewe - I Gave My Life For Thee
1. Nilikupa wewe, damu ya moyoni,
Ili wokolewe, winuke ufuni.
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
Nimekunyima ni wewe? Umenipa nini?
99. Twende kwa yesu - Come To the Saviour, Make No Delay
1. Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni; na mwenyewe, hapa asema njoo!
Na furaha tutaiona, myoyo iki takasa sana;
Kwako mwokozi, kuonana, na milele kukaa.
2. "Wana na waje," atwambia furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii, njoni.
3. Wangojeani? Leo yupo: sakiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana, njoo.
100. Kuwatafuta - Seeking The Lost
1. Kuwatafuta wasioweza, kuomba wamrejee Yesu,
Kuwaambia maneno yake "Njooni kwangu, nawapenda."
Nitakwenda (Nitakwenda) niwatafute wapotevu (Wapotevu) wageuke,
Waingie (Waingie) katika zizi la Mwokozi (la mwokozi) Yesu Kristo.
2. Kuwatafuta wasioweza, waonyeshwe Mwokozi wetu,
Kuwaongoza, wapate wote uzima ule milele.
3. Kazi hiyo nataka kufanya, leo nimesikia mwito
Kuwainua waangukao, waletwe kwake Yesu Njia.
N yimbo za kristo 81-90
81. Siku Sita Zimepita - Another Six Days' Work
1. Siku sita zime pita, Sabato tena karudi;
Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.
3. Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;
Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.
4. Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko
Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.
82. Ni Siku Ya Furaha - O Day Of Rest
1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.
2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.
3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.
83. Ewe Skuli Ya Sabato - Sweet Sabbath School
1. Ewe skuli ya Sabato,
U pazuri sana;
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.
Sabato . . . ni nzuri . . .
Sabato . . . ni nzuri . . .
Moyo wangu wanivuta,
Nije kwako leo.
2. Moyo wangu mpotovu,
Hapa una raha;
Ndipo nimwonapo Yesu,
Nije kwako leo.
3. Hapa Yesu mwenye pendo
Aniita pole:
Nimtolee moyo Yeye,
Nije kwako leo.
84. Ikumbuke Sabato - Don't Forget the Sabbath
1. Ikumbuke kote Sabato ya Bwana,
Siku tamu na bora, kupita nyingine;
Yatuletea raha, na furaha kweli,
Mwanga wake hungaza, urembo wa Yesu.
Karibie, karibie, Sabato tamu;
Karibie, Yesu pia, Bwana wa raha.
2. Itakase kweli, ukamsifu leo,
Yeye aliye sema "Mimi ndiye njia";
Nasi tukimfuata mkombozi hapa.
Atatunywesha tele maji ya uzima.
3. Siku ya nderemo! Tupishe wakati,
Tukimwimbia Yesu Rafiki Mpendwa;
Mponya wetu leo, U mwema ajabu!
Ukae kwetu, Bwana, moyoni daima.
85. Salama Tumepita - Safely Through Another Week
1. Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.
2. Utupe nuru leo toka hazina yako;
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.
3. Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
Utamu tusikize, wa raha ya milele:
4. Injili yako leo, ishike wenye dhambi;
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.
86. Ukaribie Tena - Welcome, Welcome, Day of Rest
1. Ukaribie tena, ewe siku ya raha;
Roho yakusalimu kama mwanga wa mbingu.
2. Raha yako tulivu, yafurahisha moyo;
Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.
3. Ee siku takatifu, sifa na maombi,
Na kutuhekimisha., baraka yako kubwa.
87. Siku Ya Sabato - Thy Holy Sabbath Lord
1. Siku ya Sabato, siku takatifu,
Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.
2. Ulitakasa, uliibariki,
Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.
3. Nasi tubariki tukikuabudu,
Katika siku ya raha, siku yako Bwana.
4. Halafu mbinguni, pamoja na Wewe.
Tunataka kuzishika Sabato za Bwana.
88. Siku Hii Ya Sabato - How Sweet Upon This Sacred Day
1. Siku hii ya Sabato, Tamu kufikiri
Juu ya Mungu na Mbingu Kuacha dunia.
2. Tamu kusikia Neno Toka mhubiri
Anayefundisha toba, Tupate uzima.
3. Katika vita na dhambi, Ikiwa twashindwa,
Yeye atatupa nguvu Aonaye moyo.